Tuesday 7 April 2015

GAIDI MTANZANIA SHAMBULIZI LA GARISA NI MWENYEJI WA MWANGA


Taarifa zinazoendelea kutolewa na vyombo vya usalama vya Kenya zimesema Rashid Charles Mberesero aliyekamatwa kuhusika na shambulizi la kigaidi lililofanywa na wapiganaji wa kikundi cha Al-Shabab kwenye chuo kikuu cha Garisaa ambapo watu 148 wameripotiwa kuuawa, anatokea Usangi katika wilaya ya Mwanga mkoa wa Kilimanjaro.


Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya amesema kwamba Rashid alikamatwa akiwa amejificha juu ya dari la moja ya majengo ya chuo cha Garissa ambapo baada ya uchunguzi ilidhihika kuwa hakuwa mwanafunzi wala mkaazi katika chuo hicho. Pia alipokamatwa alipatikana akiwa na mabomu kadhaa ya milipuko.
Kufuatia taarifa hizi Mbunge wa Mwanga ambaye pia ni Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe alisema “Nimeshtushwa sana na taarifa hizi. Ninaufahamu ukoo wa Mberesero ambao wanafamila wake wengi ni wakristo. Kwa wakati huu ni vyema tukaviachia vyombo vya usalama kufanya uchunguzi wa kina kuhusu suala hili.”

Dar 24.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!